Jumamosi 6 Juni 2026 - 13:43
Njia sita za kukabiliana na vita mchanganyiko vya adui katika ujumbe wa mwisho wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qum alisema: Adui ameielekeza nguvu yake katika maeneo mawili nyeti na ya kimkakati, na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ametoa njia sita za kukabiliana nayo ambazo sote tunapaswa kuzizingatia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi katika khutba ya Swala ya Ijumaa ya tarehe 15 Khordad 1405 (5 June 2026) iliyofanyika katika Msikiti wa Musalla Quds wa Qum Iran, alisema: Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei katika ujumbe wake katika mnasaba wa kumbukumbu ya kufariki kwa Imam Khomeini (r.a.), alifumbua kwa maelezo sahihi na yenye kupenya kitendawili cha vita mchanganyiko vya adui, yeye, kwa kuashiria hila chafu za adui, alitambua maeneo mawili nyeti na ya kimkakati ambayo adui amezielekeza nguvu zake zote:

Kwanza: Uwezo wa kustahimili

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Uwezo wa kustahimili unamaanisha uwezo wa jamii na uimara wake mbele ya mashinikizo, vitisho, mishtuko ya kiuchumi na mengineyo, adui anajua kwamba ikiwa watu wataondoka katika uwanja, wakapoteza matumaini yao, na subira pamoja na uwepo wao wa kijamii ukapungua, basi ngome kubwa zaidi ya ulinzi wa mfumo itaanguka.

Pili: Mfumo wa mahesabu wa viongozi

Alisema: Mfumo wa mahesabu wa viongozi unamaanisha mfumo wa kufanya maamuzi, kupanga vipaumbele, na kuwa na tathmini sahihi kuhusu vitisho na fursa. Adui anajaribu kuwafanya viongozi wetu waangukie katika makosa ya kimkakati, kama vile kukuza vitisho vya adui kupita kiasi, kudharau uwezo wa ndani, kufanya maamuzi ya haraka haraka, kuwa wanyonge mbele ya migogoro na mengineyo.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum alisema: Wakati viongozi wanapoingia katika makosa, hakuna jambo sahihi linaloweza kutekelezwa kwa utaratibu. Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei alitoa njia sita za kuzifanya hila na mipango mibaya ya maadui isiwe na athari:

1. Kusimama kidete (Muqawama)
2. Uoni wa wazi na basira katika kutambua uvumi dhidi ya ukweli, kupenya dhidi ya kutokupenya, mpango wa adui dhidi ya kosa la rafiki
3. Umoja wa Ummah mbele ya vitisho vya nje
4. Mshikamano wa taasisi za nchi
5. Kuwepo, kuhifadhi na kuaminiana kati ya watu na viongozi
6. Kutoafikiana matakwa na adui

Aliendelea kusema: Ghadir ni kuifanya upya ahadi na ukweli wa Wilayah katika nyakati ngumu zaidi, Ghadir si tu ngome salama ya Mashia, bali pia ni ngome salama ya Waislamu na hata ya wanyonge wa dunia, wakati Mtume Mtukufu (saww) alipoinua mkono wa Imam Ali (as) katika Ghadir, alitangaza kwamba njia ya uadilifu inamhitaji kamanda shujaa anayevunja safu za maadui.

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea: Leo bai'a yetu kwa Imam Mahdi (aj) kufuatia tukio la Ghadir ina maana kwamba; mbele ya matwaghuti wa zama hizi, si tu kwamba tunasikiliza amri ya Naibu wake wa haki na Faqihi Kiongozi wetu, yaani Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, bali bai'a yetu kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ndiyo bai'a ile ile tuliyompa Imam Ali (as) Ghadir Khum; kwa sababu Wilayat al-Faqih imefafanuliwa chini ya Wilayah ya Maimamu (as).

Aliongeza kuwa: Kuuawa kishahidi kiongozi wa mapinduzi ni hasara kubwa, lakini bai'a kwa uongozi wa sasa wa mapinduzi ni kuhamishwa kwa jukumu la uongozi wa Ummah kutoka kwa Hujjah mmoja kwenda kwa Hujjah mwingine, kwa sababu hiyo tunamwambia Imam Ali (as): kama tulivyofanya nawe ahadi Ghadir ya kusimama imara katika njia ya Wilayah ya haki, leo pia tunafanya ahadi na Faqihi Kiongozi na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya kuilinda Uislamu na nchi yetu, ili kama Qur'ani ilivyosema:

Shirika la Habari la Hawza,

"Na wapigeni vita mpaka pasiwepo fitna na dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu."

Msimamizi wa Haram tukufu ya Bibi Fatima Maasuma (as) alisisitiza: Tunaichukulia Ghadir ya zama hizi kuwa ni Ghadir ya wajibu; kwa hiyo tulifanya bai'a na Imam Ali (as), na tutaendelea kuwa pamoja naye, na nyuma ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi tutaendelea hadi ushindi wa mwisho.

Akikumbushia tukio la tarehe 15 Khordad na mashahidi wa harakati ya tarehe 15 Khordad ndani ya Qum na miji mingine, alisema: Tarehe 15 Khordad ina maana ya kuzalisha harakati kutoka ndani ya moyo uliofungamana na imani, leo katika mazingira nyeti ya nchi na baada ya matukio ya hivi karibuni, tarehe 15 Khordad inamaanisha usimamizi wa busara wa migogoro.

Ayatullah Saeedi akirejelea kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Shahidi Ayatullah Saeedi alisema: Yeye katika utawala wa Shah alipambana peke yake dhidi ya wawekezaji wa Marekani, akafungwa gerezani na akauawa kishahidi chini ya mateso, kisha akazikwa katika Wadi al-Salam ya Qum. Alikuwa mpiganaji mwenye basira na mfafanuzi wa ukweli, kupambana na wawekezaji wa Marekani ilikuwa vita vya kimkakati, na mapambano ya Shahidi Saeedi dhidi ya Marekani yalikuwa kimsingi ni mapambano dhidi ya mizizi ya ukoloni.

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea: Shahidi Ayatullah Saeedi alikuwa akiheshimiwa na kupendwa na Imam Khomeini (r.a.). Siku moja Shahidi Saeedi aliuambia utawala wa Shah, ambao ulikuwa umemtishia kumuua, akisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, ikiwa mtaniua na damu yangu mkaimwaga ardhini, mtalikuta jina la Khomeini katika kila tone la damu yangu.”

Akitoa pongezi kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Imam Musa al-Kadhim (as), alisema: Lakabu ya Kadhim inaonyesha kwamba yeye ni mtawala wa subira. Kadhm ina maana ya sanaa ya kugeuza hasira kuwa nguvu, Mwenyezi Mungu amesema katika Aya ya 134 ya Sura Aal Imran:

«الَّذِینَ یُنْفِقُونَ فِی السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْکَاظِمِینَ الْغَیْظَ وَالْعَافِینَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّهُ یُحِبُّ الْمُحْسِنِینَ»

“Wale wanaotoa katika hali ya faraja na dhiki, na wanaozuia hasira zao, na wanaowasamehe watu; na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.”

Mwenyezi Mungu katika aya hii ameitambulisha sifa ya kuizuia hasira si kwa maana ya udhaifu, bali kama moja ya sifa za wachamungu na watu wa Peponi.

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea: Mtu anaezuia hasira yake ili baadaye aigeuze kuwa msamaha na kisha kuwa ihsani, anamaanisha kugeuza nguvu hasi (hasira) kuwa nguvu ya kujenga, yaani kumuongoza adui, Kaadhim katika mwenendo wa Imam wa saba (as) ina maana ya kusimamia hasira ili kufikia lengo.

Ujumbe wa aya hii na mwenendo wa Imam wa saba (as) ni kwamba; katika kilele cha migogoro, mtu hatakiwi kuwa mwenye kutikisika wala kuvunjika moyo. Tunapaswa kubaki imara na wenye subira katika migogoro yote kwa kushikamana na Qur’ani na Wilayah, leo watu wetu na viongozi wetu wanahitaji basira na subira ya Kaadhim.

Akirejelea Siku ya Mubahala alisema: Tukio la Mubahala lilikuwa ni makabiliano ya Mtume (saww) na Wakristo wa Najran kwa ajili ya kuthibitisha haki na Tawhid, katika tukio hilo, Ahlul-Bayt (as), kwa mujibu wa amri ya Qur’ani, walikuja pamoja na Mtume (saww) katika uwanja ili kufanya Mubahala na Wakristo wa Najran, yaani kumuombea laana muongo.

Wakristo wa Najran walipoona nuru, yakini na ushujaa wa Ahlul-Bayt (as), waliogopa kukabiliana nao na wakakubali kulipa kodi ya Jizya; lakini kwa sababu ya ukaidi na kiburi hawakukubali Uislamu.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum, huku akisema kwamba tukio la Mubahala ni miongoni mwa nyakati zinazotikisa na zinazotia matumaini zaidi katika historia ya Uislamu, alisema: Ubeberu wa dunia ni sura halisi ya Wakristo wale wa Najran wa zama za Mtume (saww).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha